Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI CHUMI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CHINA


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (Mb.) amefanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian katika Ofisi Ndogo za Wizara leo tarehe 18 Novemba, 2024 jijini Dar es Salaam.


Mazungumzo ya viongozi hao yameangazia ushirikiano wa kihistoria na wa kidiplomasia baina ya Tanzania na China ambapo wameahidi kuendelea kuimarisha na kukuza ushirikiano uliopo kwa maslahi ya pande mbili.


Mhe. Chumi ameeleza kuwa Tanzania inafurahishwa na hatua za ushirikiano zilizofikiwa hususan kwa nchi hizo mbili kuwa na ziara za viongozi wa ngazi za juu ambazo zimeendelea kustawisha ushirikiano na kuweka mikakati mbalimbali ya kukuza ushirikiano huo.


‘’Tunashukuru kwa ushirikiano mnaotupa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo uboreshaji wa miundombinu hususan maboresho ya ujenzi wa reli ya TAZARA ambayo ni kiungo muhimu katika kuiunganisha Tanzania na nchi jirani ambazo hutumia bandar

Post a Comment

0 Comments