TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA UCHAGUZI MKOA WA SHINYANGA NA SIMIYU

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi mkuu 2025 kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 21,2025

NA NEEMA NKUMBI -  SHINYANGA

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeanza kutoa mafunzo maalum kwa waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo, maafisa uchaguzi na maafisa ununuzi kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu.

Akifungua mafunzo hayo Mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi , Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mheshimiwa Jacobs Mwambegele, amesema Tume inawategemea washiriki hao kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa weledi na kwa kuzingatia misingi ya Katiba, Sheria, Kanuni na Miongozo ya Uchaguzi katika kipindi chote cha utumishi wao hadi kukamilika kwa uchaguzi mkuu.

“Dhamana mliyopewa ya kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ni kubwa, nyeti na muhimu kwa mustakabali wa Taifa letu, Hivyo, Tume inatarajia ufanisi mkubwa kutoka kwenu,” amesema Jaji Mwambegele.

Ameeleza kuwa uchaguzi ni mchakato wa kikatiba na kisheria wenye hatua mbalimbali ambazo zinahitaji kufuatwa kwa umakini ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, wa haki na wa amani.

“Kuweni makini na mabadiliko ya sheria yaliyofanyika mwaka huu kuhusu uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Epukeni kufanya kazi kwa mazoea,” amesisitiza.

Jaji Mwambegele amewakumbusha washiriki kusoma na kuelewa vyema Katiba, Sheria, Kanuni, miongozo na maelekezo yanayotolewa na Tume ili kuepuka changamoto katika utekelezaji wa majukumu yao.

Aidha, amesisitiza ushirikishwaji wa vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kwa kuzingatia sheria, Amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza malalamiko na kuimarisha uaminifu wa mchakato mzima wa uchaguzi.

“Shirikisheni vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili katika hatua zote za uchaguzi. Epukeni kuwa chanzo cha malalamiko,” amesema.

Kwa upande mwingine, amesisitiza umuhimu wa kufanya utambuzi wa vituo vya kupigia kura mapema, kuajiri watendaji wenye sifa stahiki na kuhakikisha vifaa vya uchaguzi vinawafikia wakuu wa vituo mapema kabla ya siku ya uchaguzi.

“Ajira za watendaji wa vituo zifanyike kwa kuzingatia weledi, uzalendo na uadilifu, na siyo kwa upendeleo kwa ndugu na jamaa,” ameongeza.

Pia, amesisitiza kuwa taarifa zote za uchaguzi zitatolewa na Tume tu, na iwapo kuna haja ya kutoa taarifa nyingine, basi kibali kipatikane kutoka kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.

Jaji Mwambegele amewakumbusha washiriki kuhusu Kifungu cha 20 cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya Mwaka 2024, kinachoweka wazi kuwa mtumishi aliyeajiriwa, aliyeteuliwa au aliyeazimwa na Tume, ni mtumishi wa Tume kwa kipindi chote atakapokuwa anatekeleza majukumu ya Tume.

“Kuanzia siku ya uteuzi wenu, nyinyi ni watumishi wa Tume na mnatakiwa kuwajibika kwa Tume pekee, Msiwajibike kwa mamlaka nyingine, isipokuwa kwa mujibu wa sheria,” amesisitiza.

Mafunzo haya yanayofanyika mkoani Shinyanga yamejumuisha washiriki 83 kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu. Mafunzo hayo yameanza leo Julai 21 na yanatarajiwa kuhitimishwa Julai 23, 2025.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 21, 2025. Mafunzo hayo yamefanyika mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 21, 2025. Mafunzo hayo yamefanyika mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi mkuu 2025 kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 21,2025
Washiriki wa mafunzo hayo ambayo yanawajumuisha waratibu wa uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo kutoka majimbo yote ya Mikoa ya Shinyanga na Simiyu.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Cyprian Mbugano akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ambapo pia alitoa mada.

Hakimu mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Goodselda Kalumuna akitoa maelezo kabla ya kuwaapisha washiriki hao wa mafunzo kwa watendaji wa Uchagzi Mkuu ambapo aliwaongoza kula kiapo cha kujitoa uanachama na kutunza siri wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao ya Uchaguzi.
Washiriki wamafunzo kutoka Shinyanga na Simiyu wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na kutunza siri.
Washiriki wamafunzo kutoka Shinyanga na Simiyu wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na kutunza siri.
Washiriki wamafunzo kutoka Shinyanga na Simiyu wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na kutunza siri.
Washiriki wamafunzo kutoka Shinyanga na Simiyu wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na kutunza siri.
Washiriki wa mafunzo hayo ambayo yanawajumuisha waratibu wa uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo kutoka majimbo yote ya Mikoa ya Shinyanga na Simiyu.

Post a Comment

0 Comments