WATENDAJI WA UCHAGUZI MKUU WATAHADHARISHWA MATUMIZI YA 'MAGROUP YA WHATSAPP'

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025.

NA NEEMA NKUMBI -SHINYANGA 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji Jacobs Mwambegele, ametoa tahadhari kwa watendaji wa uchaguzi kuhusu matumizi holela ya makundi Sogozi ya WhatsApp, akisisitiza umuhimu wa weledi, uaminifu na umakini katika utoaji wa taarifa kipindi hiki nyeti cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Akizungumza leo Julai 23, 2025, wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa Watendaji wa Uchaguzi kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mwambegele amesema ni vyema Watendaji wa uchaguzi wakawa waangalifu na kuepuka matumizi holela ya makundi Sogozi ya WhatsApp.

"Hivi sasa kuna makundi sogozi ya WhatsApp, niwatahadharishe kwamba katika kipindi hiki myapunguze ili msije kukosea kutuma taarifa ya aina yoyote katika makundi hayo ambayo haikutakiwa kutumwa huko" amesema Mhe. Jaji Mwambegele.

Aidha, amesema watendaji wa uchaguzi wana wajibu wa kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kwa lengo la kuwahabarisha wananchi na wadau wa uchaguzi.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa ni lazima watendaji hao wahakikishe taarifa zinazotolewa zimesahihishwa na kujiridhisha kabla ya kuzitoa kwa umma, ili kuepusha taharuki isiyo ya lazima.

"Katika utekelezaji wa majukumu yenu mtapaswa kutoa taarifa mbalimbali kwenye vyombo vya habari ili kuwajulisha wananchi na wadau mambo mbalimbali ya uchaguzi. Nitumie fursa hii kuwasihi kwamba , iwapo kutakuwa na uhitaji wa kutoa taarifa jiridhisheni kwanza na ikiwezekana washirikishe wenzako kabla hujatoa taarifa.

Hakikisheni mnajiandaa kabla ya kukutana na vyombo vya habari. Pima taarifa yako unayotaka kuitoa kabla hujaitoa ili kuepuka kuleta taharuki badala ya utulivu katika eneo lako na taifa kwa ujumla",ameongeza Mhe. Jaji Mwambegele.

Mhe. Jaji Mwambegele pia amewakumbusha watendaji hao kuhusu umuhimu wa kutekeleza kwa wakati wajibu wa kisheria wa kubandika mabango ya uchaguzi, matangazo, orodha ya wapiga kura na taarifa nyingine muhimu kwa mujibu wa kanuni na kalenda ya uchaguzi, ili kuondoa malalamiko ya ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi.

Mwenyekiti wa Mafunzo hayo, Faustine Lagweni, amesema watendaji hao wamepatiwa mafunzo mahsusi yanayowajengea uwezo wa kitaaluma na kuwapa mwongozo sahihi wa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

"Tunakwenda kusimamia uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani. Ni lazima tuzingatie sheria, kanuni, taratibu pamoja na maelekezo yote kutoka Tume ya Uchaguzi. Uaminifu na uzingatiaji wa weledi katika kila hatua ya mchakato wa uchaguzi ni jambo lisiloepukika," amesema Lagwen.

Mafunzo hayo ya siku tatu, yaliyoanza Julai 21, 2025, yalihusisha Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa, Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa uchaguzi wa Majimbo, Maafisa Uchaguzi na Maafisa Manunuzi, ikiwa ni sehemu ya maandalizi muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025.

Post a Comment

0 Comments