Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ELIMU YA UDEREVA ZITCO YATAJWA KUZALISHA MADEREVA BORA KAHAMA

 





Elimu ya Udereva ZITCO Yatajwa Kuzalisha Madereva Bora Kahama




Na Neema Nkumbi, Kahama

Wanachuo wa shule ya udereva ya ZITCO wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wamesema elimu ya udereva waliyoipata itawasaidia kuwa madereva bora, wa kuzingatia sheria na udereva wa kujihami wanapokuwa barabarani.

Akizungumza kwa niaba ya wanachuo wenzake, Frank Emanuel amesema mafunzo waliyoyapata yamewajengea uelewa mpana kuhusu alama za barabarani, sheria na kanuni za usalama barabarani pamoja na udereva wa kujihami, jambo litakalowasaidia kupunguza ajali na kulinda maisha yao pamoja na ya watumiaji wengine wa barabara.

Amesema elimu hiyo imewajengea nidhamu, uwajibikaji na uelewa sahihi wa matumizi ya barabara, hivyo kuwaandaa kuwa madereva mahili na salama.

Mkurugenzi Mwenza wa chuo hicho, Idsam Mapande, amesema shule ya udereva ya ZITCO ilianzishwa mwaka 2019 kwa lengo la kuzalisha madereva mahili, na tangu kuanzishwa kwake imeendelea kufanya vizuri.

Mapande amesema chuo hicho huandikisha wanafunzi zaidi ya 20 kila mwezi, huku wanachuo 16 wakihitimu leo baada ya kukamilisha mafunzo yao kwa mafanikio.

Ameongeza kuwa kutokana na ubora wa mafunzo yanayotolewa, chuo cha ZITCO kimefanikiwa kushika nafasi ya pili kimkoa na nafasi ya kwanza wilayani Kahama, hali inayoonesha ufanisi na uaminifu wa chuo hicho kwa jamii.

Ametoa wito kwa vijana na wananchi kwa ujumla kukimbilia fursa ya mafunzo katika chuo hicho ili kujifunza kutambua alama na sheria za barabarani, udereva wa kujihami, na hatimaye kuwa madereva bora na wa kuaminika.

Mkurugenzi wa chuo hicho Hassan Simba ametoa ofa kwa wanachuo watakao jiunga na chuo hicho kwa punguzo la asilimia 20% pia kwa wanaotoka nje ya wilaya ya Kahama mabweni yapo na hawatachangia chochote.

Shule ya udereva ZITCO ipo Nyahanga, karibu na Shule ya Msingi Nyahanga, Wilayani Kahama.

Kwa mawasiliano zaidi, piga 0752269495 au 0766685308.

NYOTE MNAKARIBISHWA.

Post a Comment

0 Comments