Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DKT. TULIA ACKSON ATEMBELEA BANDA LA TANZANIA ISTANBUL, APONGEZA MAANDALIZI YA MKUTANO WA 153 WA IPU ARUSHA 2026


Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge Mstaafu, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) ametembelea Banda la Tanzania wakati wa maandalizi ya Mkutano wa 152 wa Umoja huo utakaofanyika Aprili 15 hadi 19, 2026 Jijini Istanbul, Uturuki.


Banda hilo ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani unaotarajiwa kufanyika Jijini Arusha, nchi Tanzania tarehe 5 hadi 9 Oktoba 2026.


Mhe. Tulia amepongeza kwa maandalizi mazuri yanayoendelea kufanyika kuelekea Mkutano huo ambao unatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki wapatao 2,000 kutoka Mabunge 183 wanachama wa IPU.


Viongozi wengine waliotembelea banda hilo ni Katibu Mkuu wa IPU, Mhe. Martin Chungong.

Post a Comment

0 Comments