
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limepokea cheti cha pongezi kwa kudhamini Kongamano la Kimataifa la Maendeleo ya Sekta ya Habari pamoja na Kikao Kazi cha Maafisa Habari wa Serikali.
Cheti hicho kimetolewa leo tarehe 21, Juni 2024 na Waziri wa Habari na Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye (Mb) wakati wa kufunga mafunzo ya Kikao Kazi cha Maafisa Habari wa Serikali.
Mafunzo hayo ya siku tano yalikuwa na lengo la kujengeana uwezo kwa maafisa Habari wa Serikali pamoja na Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari ilikuwa na kauli mbiu isemayo “Jenga mustakabali endelevu kwenye sekta ya habari katika zama za kidijiti.”
Kongamano hili liliandaliwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kongamano hilo alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
0 Comments