Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA BUNGE YA SHERIA YATEMBELEA KONGANI YA BUZWAGI NA KUPONGEZA BARRICK KWA KUFUNGA MGODI KITAALAMU

     

Wabunge kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakitembelea maeneo mbalimbali walipofanya ziara ya kikazi ya kujionea maendeleo ya Kongani Maalum la Uwekezaji (BSEZ) ya Buzwagi ambayo ipo ndani ya mgodi wa Barrick Buzwagi ambao upo katika hatua za mwisho za ufungaji.
Wabunge kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakitembelea maeneo mbalimbali walipofanya ziara ya kikazi ya kujionea maendeleo ya Kongani Maalum la Uwekezaji (BSEZ) ya Buzwagi ambayo ipo ndani ya mgodi wa Barrick Buzwagi ambao upo katika hatua za mwisho za ufungaji.
Wabunge kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakitembelea maeneo mbalimbali walipofanya ziara ya kikazi ya kujionea maendeleo ya Kongani Maalum la Uwekezaji (BSEZ) ya Buzwagi ambayo ipo ndani ya mgodi wa Barrick Buzwagi ambao upo katika hatua za mwisho za ufungaji.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Utawala , Katiba na Sheria ya Bunge , Dkt Damas Ndumbaro akizugumza na wajumbe wa kamati hiyo , kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya kahama , viongozi wa halmashauri ya Kahama na wafanyakazi na menejimenti ya Barrick Buzwagi wakati wa ziara hiyo ya siku moja ya kutembelea kongani maalum la uwekezaji ya Barrick Buzwagi.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji , Dkt. Pius Chaya akiongea na Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria walipofanya ziara ya kikazi ya kujionea maendeleo ya Kongani Maalum la Uwekezaji (BSEZ) ya Buzwagi ambayo ipo ndani ya mgodi wa Barrick Buzwagi ambao upo katika hatua za mwisho za ufungaji.
Meneja wa Ufungaji wa Mgodi wa Barrick Buzwagi , Mhandisi Zonnastraal Mumbi akizungumza mbele ya Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria walipofanya ziara ya kikazi ya kujionea maendeleo ya Kongani Maalum la Uwekezaji (BSEZ) ambalo lipo ndani ya mgodi wa Barrick Buzwagi ambao upo katika hatua za mwisho za ufungaji.
Mkurugenzi Mkuu wa TISEZA,Gilead Teri akizungumza mbele ya Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria walipofanya ziara ya kikazi ya kujionea maendeleo ya Kongani Maalum la Uwekezaji (BSEZ) ambalo lipo ndani ya mgodi wa Barrick Buzwagi ambao upo katika hatua za mwisho za ufungaji.

***
# Kamati ya Bunge ya Sheria yaitaka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum (TISEZA) kuisimamia Kongani hiyo badala ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.

Kamati ya kudumu ya Bunge Utawala , Katiba na sheria imeelekeza serikali kupitia Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kuikabidhi rasmi kwa ajili ya kusimamiwa Kongani Maalum ya Uwekezaji ya Buzwagi (BSEZ) kwa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum Tanzania (TESIZA) ili kuhakikisha inaendelea kuvutia wawekezaji na kutengeneza mazingira mazuri ya biashara ili kuleta matokeo Chanya pia imepongeza Barrick kwa kufunga mgodi kitaalamu .


Akizungumza kwenye majumuisho ya ziara ya kamati hiyo , Mwenyekiti wake , Dkt. Damas Ndumbaro (MB) amesema kamati imeonelea kwamba ni muhimu kwa mamlaka ya uwekezaji kusimamia kongani hiyo badala ya kuikabidhi kwa halmashauri ya Manispaa ya Kahama.

“Tunachukua fursa hii ya kipekee kwanza kwa kuwashuruku uongozi wa Barrick kwa kazi nzuri ya ufungaji wa mgodi huu wa Buzwagi kitaalamu na kuweka mazingira mazuri ya uanzishwaji wa kongani maalum ya biashara na uwekezaji ni jambo muhimu kwa maslahi ya nchini yetu,”

“Tumetembelea eneo hili mahususi kwa ajili ya uwekezaji tumeona wenyewe kwamba maji, miundombinu ya barabara , umeme vipo ambavyo ni kichochea cha kuvuta uwekezaji wa ndani na wa nje,” amesema Dkt. Ndumbaro.

Ameongeza kwamba kwenye mchakato wa kuvutia wawekezaji nchini moja ya changamoto ni sheria ya fedha ambayo kwa namna fulani si rafiki sana kwa kuvutia wawekezaji tutaendelea na kuishauri serikali na mapendekezo yetu ni baadhi ya vifungu vya sheria ya fedha viondolewe ili kufungua milango zaidi ya uwekezaji.

Dkt. Ndumbaro amesisitiza kuwa ni muhimu kwa Halmashauri ya Kahama kuendelea na shughuli zingine za wananchi na kuiachia Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) kwenye uendelezaji wa kongani hii na kuvutia wawekezaji nchini.

Dkt. Ndumbaro amesema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inaelekeza kila wilaya kuwa na kongani ya viwanda ili kuongeza ajira kwa wananchi na kukuza uchumi wa maeneo husika. 

Ameitaka pia (TISEZA) kuwa karibu na eneo hilo na kulitangaza zaidi ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi ndani ya nchini na nje.

“Kupitia Ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ni lazima serikali iendelee kuutia wawekezaji wa ndani na wa nje ili kupunguza tatizo la ajira na kupanua wigo wa mapato ya serikali nchini,” ameongeza Dkt. Ndumbaro.

Amesema kongani hiyo ni ya kipekee ikilinganishwa na maeneo mengine ya uwekezaji kwa kuwa ina miundombinu muhimu ikiwemo umeme wa uhakika, maji ya kutosha, barabara pamoja na uwanja wa ndege unaorahisisha usafiri wa wawekezaji.

“Tunataka TISEZA wawe karibu na kongani hii ili wawekezaji watakapopatikana wasikumbane na changamoto za kiutaratibu katika hatua za kuanzisha uwekezaji wao,” amesema Dkt. Ndumbaro.

Kwa upande wake , Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji , Dktt. Pius Chaya amesema kuwa, serikali imeyachukua mapendekezo ya kamati ya kudumu ya Bunge kuhusu mamlaka ya uwekezaji kusimamia kongani hiyo badala ya halmashauri ya kahama kwa ajili ya kuongeza ufanisi.

Amefafanua kwamba serikali ya awamu ya sita kwa kushirikiana na sekta binafsi , kama vile Barrick itaendelea na mipango hiyo ambayo ipo kwenye dira ya taifa ya maendeleo 2020-2050 ili kuhakikisha tunaendelea kupunguza umasikini na kukuza uchumi wa nchini.

“Kupitia mpango wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali (PPP) tunataka mchango wa sekta binafsi kwenye pato la taifa lifike 70% ili kuendelea kufungua milango zaidi ya ushirikishwaji wa sekta hiyo muhimu kwenye nguzo za uchumi wa nchini yetu,” ameongeza Dkt. Chaya

Amesema serikali inaipongeza Barrick ambayo ina ubia nayo kupitia kampuni ya Twiga Minerals kwa kuendelea kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo na kuahidi kwamba ushirikiano huo utaendelea ili kufungua fursa zaidi na kupanua mazingira wezeshi ya uwekezaji hapa nchini.

Naye, Meneja wa Ufungaji wa Mgodi wa Buzwagi Zonnastraal Mumbi amesema Barrick itaendelea kushirikiana na serikali katika kuvutia wawekezaji kwa kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji na kuzingatia viwango vya kimataifa vya ufungaji wa mgodi na weledi.

“Mgodi wa Barrick Buzwagi ulianza mchakato wa ufungaji 2021 kwa kushirikiana na Tume ya Kitaifa ya Ufungaji na baadaye tukaanza rasmi safari ya kubadilisha eneo hili ilikuwa sehemu ya uwekezaji wenye tija baada ya kujiridhisha pamoja na serikali kwamba miundombinu ya hapa ni bora na ya kuvutia uwekezaji,” amesema.

Mhandisi  Magige Marwa kutoka Mamlaka ya Maji Safi wa Mazingira Kahama (KUWASA) akizungumza na kamati hiyo ilipotembelea mradi wa ujenzi wa chujio la maji la Mwendakulima ambayo unatazamiwa kuhudumia zaidi ya 66% ya wakazi waishio Manispaa ya Kahama na ina uwezo wa kutoa lita milioni 10 kwa siku.

“Mradi huu unatarajiwa kukamilika Mwezi Juni mwaka huu na mpaka sasa 78% ya mradi mzima umeshakamilika kutoka na kasi ya ujenzi wa mradi huu mkubwa kwenye mji huu wa kahama,” amesisitiza.

Mhandisi Marwa amefafanua kwamba mradi huo wa chujio la maji ya mvua 62% imefadhiliwa na mgodi wa Barrick- Buzwagi na 38% ni Kuwasa kupitia Wizara ya Maji na Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Kongani ya Barrick Buzwagi ina ukubwa wa hekta 1,333 na ipo katika eneo lililokuwa Mgodi wa Barrick Buzwagi. Hadi sasa jumla ya wawekezaji 35 wameonesha nia ya kuwekeza katika eneo hilo, ambapo mwekezaji mmoja tayari ameanza uzalishaji wa vipuri na vifaa vya migodini, watano wako katika hatua za kufuatilia leseni huku wawekezaji 29 wakiwa katika hatua za awali za uwekezaji.

Post a Comment

0 Comments