Wagombea 17 wameteuliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kugombea ubunge Jimbo la Ismani lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Mkoani Iringa.
Uteuzi huo umefanywa kwa niaba ya Tume na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ismani, Ndugu. Caroline Angwen Otieno leo tarehe 10 Mei, 2026.
Wagombea walioteuliwa na vyama vyao kwenye mabano ni Ndugu. Emmanuela Kaganda Mtatifikolo (CCM), Ndugu. Farida Issa Mwapungu (MAKINI), Ndugu. Asha Athumani Chuma (UPDP), Ndugu. Protas Shaibu Mgimbila (CCK), Ndugu. Fidelis Daud Mtikile (SAU), Ndugu. Hadija Husen Makawa (ADA-TADEA) Ndugu. Zavely Raurent Seleleka (UDP) na Ndugu. Subira Majuto Kalolo (NLD).
Wengine ni Ndugu. Bernard George Mwingira (DP), Ndugu. Burton Emilyo Chetenge (NCCR-Mageuzi), Ndugu. Mbalinga Christian Thomas (N.R.A), Ndugu. Mark Isdory Mhemela (AAFP), Ndugu. Nassim Yahaya Upete (CUF), Ndugu. Mwaka Lameck Mgimwa (TLP), Ndugu. Asma Abdallah Othman (UMD), Ndugu. Maimuna Martin Lumato (ADC) na Ndugu. Daudi Issa Masasi (CHAUMMA).
Akizungumza baada ya uteuzi huo, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo, Ndugu. Caroline Angwen Otieno amesema kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Tume,
Kampeni kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Ismani pamoja na kata 12 za Tanzania Bara zitaanza kesho tarehe 11 hadi 31 Mei, 2026 na uchaguzi utafanyika siku ya Jumatatu tarehe 01 Juni, 2026.
Baada ya hatua hii ya uteuzi, kinachofuata ni kubandika fomu za uteuzi eneo la wazi kwa ajili ya kuwapa fursa ya kuweka pingamizi wale wanaoruhusiwa kuweka pingamizi kwa mujibu wa sheria.
Baada ya saa 24 kupita na endapo hakutakuwa na pingamizi wagombea hao 17 wataendelea na kampeni kuanzia kesho tarehe 11 hadi 31 Mei, 2026 na uchaguzi utafanyika tarehe 01 Juni, 2026, amesema.
Kata 12 za Tanzania Bara zitakazofanya uchaguzi mdogo wa Udiwani ni Mzimuni iliyopo Manispaa ya Kinondoni; Zongomera, Manispaa ya Kahama; Itilo, Halmashauri ya Mji wa Nzega; Ketare, Halmashauri ya Mji wa Tarime na Nyumbigwa, Halmashauri ya Mji wa Kasulu.
Nyingine ni kata ya Kala iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi; Ziba, Halmashauri ya Wilaya Igunga; Kamsisi, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele; Nyamugali, Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe; Namasakata Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru; Bwongera, Halmashauri ya Wilaya ya Chato na Kibiti Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti.



















0 Comments