Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TANZANIA KUIMARISHA UFANISI WA MFUMO WA KODI ILI KUKUZA UWEKEZAJI NCHINI


Tanzania imechukua hatua stahiki za kuimarisha ufanisi wa mfumo wake wa kodi, ili kukuza uwekezaji na biashara na mataifa mbalimbali duniani.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahamoud Thabit Kombo, amesema hayo tarehe 13 Novemba, 2024 jijini Dar es Salaam alipozungumza na Jumuiya ya Wanadiplomasia wanaowakilisha nchi na Mashirika ya Kimataifa nchini.


Mhe. Kombo amesema Serikali inatambua malalamiko yanayohusiana na mfumo wa ulipaji kodi kwa wafanyabiashara wa ndani na wa kigeni na katika kukabiliana na changamoto hiyo imeunda Tume ya Rais kwa ajili ya kupitia na kutathimini mfumo uliopo, ambapo pia itapitia upya Sera ya kodi. Ameingeza kuwa Serikali itashirikisha wadau mbalimbali ili kutoa maoni yao yatakayochangia kuleta matokeo chanya kwa walipa kodi na tija kwa Taifa.


Mhe. Kombo ameongeza kuwa, katika kuimarisha Diplomasia ya kijamii na kiuchumi na kuendana na Siasa za kImataifa,

Post a Comment

0 Comments