Balozi Luteni Jenerali Paul Mella akizungumza wakati Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 ikizungumza na Waanadishi wa Habari, amesema tukio la Oktoba 29 limetoa funzo kubwa kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama na kwamba vitakuwa vimejifunza pindi inapotaka kutokea matukio ya aina hiyo.
Amesema uchunguzi wao umebaini kuwa mamlaka za vyombo vya ulinzi na usalama vilikuwa na taarifa likini vilizidiwa kasi.
Aidha, amesema kwamba mbinu zilizotumika zilikuwa sio za kawaida, huku akieleza kuwa mipango mbalimbali ilikuwa ikipangwa kwa Teknolojia na nguvu ya Mtandao.
0 Comments